Manchester City Yatwanga Copenhagen 3-1 Ulaya
Na Mwana Wa Afrika
Manchester City imeendelea kung'ara katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya baada ya kushinda 3-1 jana usiku katika uwanja wa Parken wa Copenhagen.
De Bruyne aliongoza City dakika ya 10 kupitia ushirikiano wake na Foden. Timu hiyo inaendelea kuwa na fomu nzuri, hususan baada ya De Bruyne kurejea na kuchangia mabao mawili na kufunga moja.
Jack Grealish alilazimika kutoka kutokana na jeraha, nafasi yake ikachukuliwa na Mbelgiji Jeremy Doku dakika ya 21.
Copenhagen walijibu dakika ya 34 baada ya A. Moraes kutoa pasi ovyo. City wakaongeza la pili kupitia juhudi za De Bruyne na Bernardo Silva dakika ya 46.
Copenhagen walijaribu kurudi kipindi cha pili, lakini matumaini yalizimwa na Phil Foden dakika za lala salama baada ya De Bruyne kurudisha mkono wa kwanza na kumpa pasi.
Manchester City itawakaribisha Copenhagen nyumbani Etihad tarehe 6 Machi kwa mechi ya mkondo wa pili. Copenhagen watatakiwa kufunga magoli 3-0 ili kumtoa Pep.
Matokeo mengine ya jana: RB Leipzig 0-1 Real Madrid. Leo: Lazio vs Bayern Munich, PSG vs Real Sociedad.