Shabana FC Yapambana na Changamoto za Matokeo Mabovu na Uhamisho wa Uwanja
Na Mwana Wa Afrika
Timu ya Shabana inakabiliwa na changamoto kubwa huku ikiendelea kurekodi matokeo mabovu katika Ligi Kuu ya Kenya.
Katika mechi tano zilizopita, wameshinda mara moja, kutoka sare mara moja, na kupoteza mara tatu.
Kwa jumla, Shabana wameshacheza mechi 22, wakishinda mara 4, kutoka sare mara 6, na kupoteza mara 12. Wanashikilia nafasi ya 17 kwenye ligi wakiwa na alama 18.
Kichapo cha moja kwa bila kutoka kwa Police FC kimewaacha na hali ngumu, na sasa wamepoteza mashabiki kutokana na mwenendo wao mbaya.
Hata hivyo, hali inaweza kubadilika wanapokutana na Bandari FC tarehe 2 Machi, 2024, na KCB tarehe 9 Machi, 2024. Mashabiki wanaweza kutumaini mabadiliko kwenye matokeo ya mechi zijazo.
Kupitia uhamisho wa uwanja wao wa nyumbani kutoka Gusii Stadium kwenda Odinga uliyoko Homabay, Shabana inakabiliwa na changamoto zaidi, na hii inaweza kuathiri utendaji wao.
Ni matumaini ya mashabiki kwamba timu itaweza kurekebisha mwenendo wao na kurejesha imani ya wapenzi wao wa soka.